Wachungaji watatu wamenusurika kichapo cha mbwa koko kutoka kwa wananchi mara baada ya kushindwa kumfufua marehemu ambaye ni mwanakijiji mwenzao baada ya wachungaji hao kudai wanauwezo wa kumfufua marehemu huyo aliyefariki siku za chache zilizopita na kuzikwa katika makaburi ya kijiji hicho.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Christopher Angelo, amesema tukio hilo lilitokea Mei 7, 2018 majira ya saa 4 asubuhi .

Ambapo amesema wananchi walishikwa na hasira kubwa baada ya wachungaji hao kuwapotezea muda ambao walitumia kwa siku saba usiku na mchana kusali na kuomba bila mafanikio yeyote.

”Wananchi, ndugu na jamaa walikasirika kutokana na kuona kuwa wachungaji hao wanawatapeli na kwa sababu waliwasababishia kuingia gharama kubwa ya kulisha watu waliokuwa wakishiriki maombi hayo,” alisema.

Kwa mujibu wa Angelo, baada ya kuona hafufuki, ndugu wakiongozwa na mama mzazi wa marehemu waliamua kwenda kutoa taarifa ofisi ya kijiji, ili kuepusha vurugu ambazo zilitaka kutokea.

Mwenyekiti huyo alisema viongozi wa Kijiji baada ya kufika kwenye eneo hilo walikuta ndugu wa marehemu wakiwa wanafoka kwa hasira huku wakiwa wanawatuhumu wachungaji hao kuwa ni matapeli.

“Sisi uongozi wa Kijiji tulikuta vurugu na wananchi walikuwa wanataka kuwapiga wachungaji hao, tulichofanya kuepusha shari ni kuwaondoa wachungaji hao eneo hilo na kwa kweli walitii agizo hilo na kuondoka zao,” alisema Angelo.Chanzo- Nipashe

Mwenyekiti ameongezea kuwa wachungaji hao watatu walifika kwenye ofisi ya Kijiji na kujitambulisha kuwa wao ni wachungaji wanatoka katika Kijiji cha Nsimbo na watakuwapo kijijini hapo wakiwa wameitwa na ndugu wa marehemu, Raymond Mirambo aliyefariki dunia siku moja na kuzikwa kijijini hapo.

 

Everton yamtimua Sam Allardyce
Meek Mill amuwashia mshumaa Drake