Mashabiki wa soka nchini Brazil jana walishuhudia tukio lisilo la kawaida michezoni baada ya wachezaji tisa kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ‘Derby’ kati ya  timu za Victoria na Bahia, baada ya kutokea vurugu kuelekea mwisho wa mechi

Vurugu hizo ziliibuka zikiwa zimesalia dakika 11 kabla ya mchezo huo kumalizika baada ya mchezaji wa Bahia kusheherekea goli ambalo aliisawazishia timu hiyo na kuwa sawa kwa mabao 1 – 1.

Aidha, Kufuatia bao hilo lililofungwa kwa Penati na mchezaji wa Bahia na kushangilia kwa mtindo ambao ulionekana kuwakera wachezaji wa timu mwenyeji ambayo ni Victoria walianza kumshambulia kabla ya wenzake wa Bahia kuingilia kati kitendo ambacho kilipelekea mwamuzi kutoa kadi hizo na mchezo kuishia dakika ya 79.

Wachezaji sita wa Timu ya Victoria ambao walikuwa wenyeji walipata kadi nyekundu za moja kwa moja huku wachezaji watatu wa timu ya Bahia nao walionyeshwa kadi nyekundu hivyo kufanya mchezo huo usiendelee.

Refarii alilazimika kuahirisha mechi kutokana na taratibu za mchezo wa soka kuhitaji angalau wachezaji saba wa timu wawepo uwanjani.

Mahakama ya michezo ya Brazil inasubiriwa kuamua juu ya hatua gani za kuchukua kufuatia vurugu hizo ambazo zilipelekea kuharibika kwa mchezo huo ambapo timu zilikuwa zimefungana bao 1- 1.

Infantino kuongoza mkutano wa FIFA akiwa Tanzania
Eden Hazard aiweka njiapanda Chelsea