Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamekubaliana kwa pamoja kutoa posho zao za siku moja kwa ajili ya kuwafariji ndugu wa wanafunzi 33 wa shule ya Lucky Vincent waliofariki kwa ajali ya gari mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa Spika Ndugai, uongozi wa kambi zote mbili ulimshauri kuwa wabunge wasipewe posho zao za siku moja ili ziweze kugawanywa kwa wafiwa, kwa usawa.

Bunge lilitumia dakika moja ya ukimya (moment of silence) kwa lengo la kutoa heshima na kuwakumbuka wanafunzi, walimu na madereva waliopoteza maisha katika ajali hiyo mbaya iliyotokea wilayani Karatu.

Leo, Makamu wa Rais, Samia suluhu Hassan amengoza waombolezaji mkoani Arusha kuaga miili ya marehemu na kutoa heshima zao za mwisho.

Wanafunzi hao walipoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea Jumamosi iliyopita katika eneo la Rotya wilayani Karatu, walipokuwa wakienda kufanya mtihani wa ujirani mwema katika shule ya Tumaini Junior Academy.

 

JPM awalilia wanafunzi, asema tumewapoteza mashujaa wetu katika elimu
Tanzania ni nchi pekee barani Afrika kuwa na taasisi ya kudhibiti kemikali