Mamia elfu ya watu nchini Algeria wameingia barabarani jana kushiriki maandamano ya kudai Rais Abdelaziz Bouteflika aondoke madarakani.

Kwa mujibu wa Reuters, jana takribani watu milioni moja waliingia mtaani katika mji mkuu wa Algiers, ikiwa ni Ijumaa ya sita yenye mafanikio kwa waandamanaji hao.

Jeshi la polisi la Algeria liliwafyatulia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji walipokuwa wakikaribia kwenye makazi ya rais.

Mkuu wa majeshi, Luteni Generali, Ahmed Gaed Salah alitoa wito wa kuwepo hali ya utulivu na kusubiri kuitishwa kwa uchaguzi mkuu.

Hata hivyo, wapinzani nchini humo wameonesha kutokubaliana na wito huo wakidai kuwa wanaamini uchaguzi hautakuwa huru na haki endapo Rais Bouteflika ataendelea kuwa madarakani.

Maandamano hayo dhidi ya Rais Bouteflika yalianza mwezi uliopita kufuatia taharuki iliyoibuka baada ya rais huyo ambaye amekuwa adimu machoni kwa umma tangu aliposhambuliwa na kiharusi mwaka 2013, kutangaza kuwa atawania tena nafasi hiyo.

Kufuatia maandamano hayo, Rais huyo alitangaza kuwa hatagombea tena katika uchaguzi ujao lakini ameendelea, lakini waandamanaji wamedai kutoridhishwa na ucheleweshwaji wa uchaguzi mkuu ujao hali inayomuongezea miaka mingine ya kuendelea kutawala.

Ajifungua mapacha mwezi mmoja baada ya kujifungua mtoto wa kwanza
Nandy aachia ngoma mpya, ''Halleluyah''