Umoja wa vyama 12 visivyokuwa na uwakilishi bungeni, umekutana kwa siri kujadili mambo kadhaa ikiwamo suala la kisiasa la Rais John Pombe Magufuli kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara kwa vyama hadi 2020.

Umoja huo ambao ulikutana katikati ya wiki iliyopita kwa siku tatu mfululizo, viongozi wake wamekubaliana kutangaza msimamo wao kuhusu suala hilo septemba 28.

Mmoja kati ya wajumbe wa kikao hicho, alisema baada ya vikao hivyo watatangaza tamko zito iwapo serikali haitaondoa zuio lake ndani ya siku 14 kuanzia sasa.

“Haiwezekani kusubiri hadi 2020 kwa sababu vyama vyetu ndiyo kwanza tunatakiwa kuvijenga na sheria inaturuhusu kushiriki siasa” alisema mjumbe huyo.

Katibu Mkuu wa Chama cha SAU, Ally Kaniki wakati akifanya mazungumzo na gazeti la  Mwanachi amekiri kukutana na kukubaliana mambo kadhaa lakini amekataa kuzungumzia suala hilo kwa undani

Mbowe: JPM Kagera unaenda lini?
Jeshi la Polisi latakiwa kuwatendea haki wananchi wanyonge