Halmashauri tatu za Wilaya ya Njombe Zimetakiwa Kutoa Kipaumbele Cha Mikopo ya Vijana, Wanawake na Walemavu Kwa Wajasiliamali Wenye Vitambulisho Vya Ujasiliamali Ili Kuwakumbusha Wengine Wanaokwepa Kununua Vitambulisho hivyo.

Hayo yamesemwa Katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri ambapo amesema kuwa amefikia hatua hiyo ili kuhamasisha wajasiriamali wanaokwepa kununua vitambulisho hivyo.

”Kwasababu vitambulisho vyetu hivi ni vya wajasiriamali wadogo na halmashauri imepewa nafasi kisheria ya kutenga asilimia kumi za mapato yake, inapoona wakati wa kutoa mikopo basi hawa ambao wana vitambulisho hawana maswali tayari tunawafahamu wapo ndani ya sekta rasmi kwa hiyo wafikiliwe kwanza kuongezewa kipato ili wainuke hivi vitambulisho sio vya kudumu,”amesema Msafiri

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amepiga marufuku watendaji ambao wameendelea kuwatoza ushuru wajasiriamali wenye vitambulisho Vya wajasiriamali kwa madai kwamba wanatakiwa kuchangia baadhi ya tozo kwa kufanya hivyo kunapingana na miongozo iliyotolewa na Rais Dkt. Magufuli.

Aidha, baadhi ya wajasiriamali mjini Njombe akiwemo Michael Uhaula wakizungumzia agizo la mkuu wa wilaya wamesema hatua hiyo itawapunguzia changamoto katika kupata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa makundi hayo huku wakidai kuwa mikopo hiyo imegubikwa na wimbi la kujuana na upendeleo.

“ninaweza kusema agizo hili inaweza ikawa ni ahueni kwa wajasiriamali wadogo lakini itakuwa ni ahueni endapo kutakuwa na utaratibu maalumu kati ya mabenki na hawa wajasiriamali kwasababu mwanzoni kulikuwa na mlolongo mrefu sana kuweza kupata hii mikopo”alisema Michael uhaula

Hata hivyo, wajasiriamali hao wamelalamikia kitendo cha kuingiza siasa zaidi katika mikopo hiyo ambayo wamesema inatolewa kwa kujuana zaidi.

Video: Vigogo 7 watumbuliwa wengine matumbo moto, Ukatili wa ngono kwa watoto watikisa
Mvua yaharibu mawasiliano Kyela