Virusi vya Corona vimeendelea kuvuka mipaka katika nchi mbalimbali duniani, kuanzia China, Ulaya, Marekani na Afrika; ambapo Sudan pia imethibitisha kupata mgonjwa wa kwanza.

Serikali ya Sudan imeeleza kuwa mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 50 aliyefariki dunia Alhamisi jijini Khartoum, alikuwa na virusi vya corona.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Afya, Machi 13, 2020 imeeleza kuwa mwanaume huyo alikuwa ametembelea nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika wiki ya kwanza ya mwezi Machi.

Sudan imechukua hatua za dharura za tahadhari, ilipiga marufuku utoaji wa hati za kusafiria kwa nchi nane ikiwa ni pamoja na Italia na Misri. Hatua hiyo ilizuia pia usafiri wa basi kati ya nchi hiyo na Misri.

Misri ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuthibitisha kuwa na mgonjwa wa Virusi vya Corona. Imeshapata vifo viwili na waathirika 80 wa virusi hivyo.

 

Corona: Trump atangaza hali ya dharura, Google kutoa huduma maalum
VIRUSI VYA CORONA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuepuka, hatua za kuchukua