Viongozi watatu kati ya 10 wa Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan wametangaza kujiuzulu huku wananchi wa nchi hiyo wakiendelea na maandamano kulishinikiza jeshi likabidhi madaraka kwa raia.

Viongozi hao wa kijeshi waliojiuzulu ni Luteni Jenerali Omar Zain al-Abdin, Jalaluddin Al-Sheikh na Al-Tayieb Babikir. viongozi hao wametangaza kujiuzulu muda mfupi baada ya kufanyika mkutano kati ya wawakilishi wa jeshi na viongozi wa waandamanaji.

Baada ya mkutano huo, jeshi lilitangaza kuwa limefikia makubaliano kwa mambo mengi miongoni mwa matakwa ya waandamanaji wa pande hizo mbili ambazo ziliafikiana kuunda kamati ya pamoja ili kutatua tofauti zao.

Aidha, viongozi hao wakuu wa Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan wamejiuzulu baada ya kutuhumiwa kuwa walikuwa na ushirikiano wa karibu na utawala uliopinduliwa.

Hata hivyo, itakumbukwa kuwa, Rais Omar al-Bashir alipinduliwa mnamo Aprili 11 baada ya maandamano ya miezi kadhaa ya wananchi na hivi sasa Baraza la Kijeshi la mpito chini ya uongozi wa Luteni Jenerali Abdel Fattah al Burhan Abdelrahman limechukua madaraka kwa muda.

Umoja wa Mataifa waingilia kati hukumu ya kifo
Rais Putin kuwakutanisha Kim Jong Un na Rais Trump kuhusu Nyuklia

Comments

comments