Viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani nchini wamejichimbia visiwani Zanzibar kwa ajili ya kupatiana mafunzo mbalimbali juu ya mwenendo wa siasa na demokrasia.

Viongozi waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamadi, pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa na Kiongozi wa ACT – Wazalendo Zitto Kabwe.

Mbali na hao, viongozi wengine walionekana na Rais wa Chama Cha Mawakili Tanzania, (TLS) Fatma Karume pamoja viongozi wengine mashuhuri nchini ambapo imeelezwa walijadili juu ya mwenendo wa hali ya kisiasa nchini.

Aidha, Kaimu Msemaji wa chama cha CUF, Mbarara Maharagande amesema kuwa kikao hicho kimeandaliwa na taasisi ya Marekani IR kupitia kwa Katibu wa CUF, Maalim Seif.

“Ni kweli kuna semina inafanyika ya viongozi wa vyama inafanyika Zanzibar ambayo inafanyika kwa siku tatu, na aliyewaalika ni Katibu Mkuu wetu Maalim Seif na imeandaliwa na taasisi ya IRSA, watu wa democratic ya America,” amesema Maharagande.

Katika ukurasa wake wa Twitter Maalim Seif aliandika “ni heshima kubwa kwangu na kwa CUF kuandaa na kuwa mwenyeji wa kikao cha kutathmini demokrasia yetu na kujitathmini sisi wenyewe kama vyama vya upinzani na mwelekeo wetu.”

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 18, 2018
Mngereza aeleza alivyochangamkia mchongo wa TACIP, ‘inaongeza thamani’