Sekretrieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nchini Tanzania inatarajia kuanza kuwachunguza viongozi wa umma kutoka mikoa 12 juu ya madai ya mgongano wa maslahi kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Hayo yamesemwa na ofisi hiyo kupitia taarifa ya Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Aidha, taarifa hiyo imeitaja mikoa ambayo watumishi wa umma watafanyiwa uhakiki huo ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Geita, Kagera, Mara, Mwanza, Dodoma, Tabora, Singida, Dar es salaam na Shinyanga, huku wakitakiwa kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.

“Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma inatoa wito kwa wote ambao watahusika katika shughuli hii kutoa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo.”imesema taarifa hiyo.

Nyumba 20 zateketea kwa moto nchini Uingereza
Kanisa Katoliki lapinga vikali mapenzi ya jinsia moja

Comments

comments