Vijana nchini wametakiwa kutumia fursa zilizopo ili ziweze kuwanufaisha pia kuepukana na kukimbilia nchi za nje kwa kisingizio cha kutafuta maisha.
 
Hayo yamesemwa na Kamishina wa Polisi, Mussa Ali Mussa wakati akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani-Tanzania yaliyofanyika leo Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
 
“Vijana acheni mipango ya kwenda kuzitafuta fursa nje ya nchi kwani wenzenu kutoka nchi hizo wamekuwa wakija kunufaika nazo hapa nchini” amesema Kamishna Mussa.
 
Amesema kuwa serikali imeweka mazingira mazuri hivyo ni vizuri hali hiyo ikatumika kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo hasa katika wakati huu nchi ikiingia katika uchumi wa viwanda.
 
Hata hivyo, Katika hatua nyingine Kamishna Mussa amesema kuwa amani ya nchi itadumishwa na kila mtu na kuwa watu waondoe dhana ya kuwa amani hiyo italetwa na vyombo vya dola ikiwemo polisi.
 
  • Wawili mbaroni kwa kusafirisha madawa ya kulevya
 
Kwa upande wake Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la UN linaloshughulikia wahamiaji la IOM, Dkt. Quasim Sufi amesema kuwa amani ni jambo la muhimu kwa nchi na mustakabari wa maendeleo.
 
  • Rais Magufuli kutoa ajira 3,000
 
Maadhimisho hayo yameandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na taasisi mbalimbali

Hospitali yathibitisha kupokea fedha za mchango wa Lissu
Wagonga nyundo wa London washindwa kutamba mbele ya Spurs