Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia Chama Cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa ameungana na wabunge wanne kutoka vyama vya upinzani kumshtaki Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa lengo la kufungua mashtaka hayo mahakamani si kumtetea Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad bali ni kutetea ofisi ya mkaguzi huyo.

Amesema kuwa kama hatua hiyo iliyochukuliwa na Spika Ndugai ikiachwa, italeta misingi mibaya katika ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali.

“Tumeamua kufanya hili kwasababu ya Ofisi, hili naomba lieleweke, tunafungua mashtaka mahakamani si kumtetea Prof. Assad bali ofisi yake,”amesema Zitto

Video: Kauli ya CAG haikuwa na afya kwa Taifa letu- Wakili Manyama
Kangi Lugola ateta na UNHCR kuhusu wakimbizi

Comments

comments