Video mpya ya wimbo wa Roma alioubatiza jina la ‘Zimbabwe’ imeweka historia kwa nyimbo za hip hop kwenye mtandao wa YouTube ndani ya saa 24 tangu ilipowekwa, hususan nyimbo alizowahi kutoa.

‘Zimbabwe’ iliyoongozwa na Nicklass iliyowekwa juzi jioni imeshika nafasi ya kwanza kwenye ‘trending’ ya YouTube ikiteka vichwa vya habari na kuzunguka kwa kasi kwenye mitandao.

Ndani ya saa 24, ‘Zimbabwe’ ambayo imetambulishwa kwenye vyombo vya habari na mke wa Roma imeangaliwa zaidi ya mara 327,800, tarakimu ambazo ni nadra kwa video za nyimbo kubwa za hip hop zilizowahi kutolewa ndani ya Tanzania kwa muda huo.


Hii ni dalili ya wazi kuwa video hii inaweza kupata watazamaji milioni moja ndani ya muda mfupi na hata kuzivunja rekodi zilizowekwa na nyimbo za hip hop kama ‘Dume Suruali’ ya Mwana FA ambayo ndani ya miezi nane imeangaliwa zaidi ya mara milioni 4.

Bado Roma hajajitokeza  hadharani kuzungumzia wimbo na video hiyo kwenye vyombo vya habari lakini kiu ya mashabiki wake imezidi kuwa kubwa na huenda atakapojitokeza ataongeza kasi zaidi ya watazamaji wa video hiyo.

Ndani ya ‘Zimbabwe’ iliyopikwa na Bin Laden wa Tongwe Records, Roma amesimulia tukio la kutekwa kwa siku tatu na watu wasiojulikana na hatma yake baada ya tukio hilo.

Video: Mtoto wa mgombea TFF ashikwa chooni akitaka kutoa rushwa kwa wajumbe Dodoma
Kenyatta ampa ujumbe Raila baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Urais

Comments

comments