Kwa kawaida suala la unyoaji wa vywele au vinyweleo vya mwili hufanywa wakati mhusika akiwa ametulia na wakati mwingine kwenye maeneo ya siri. Lakini hii imekuwa tofauti kwa mwanamke mmoja, mkaazi wa jimbo la Florida nchini Marekani ambaye ameyafanya hayo akiwa anasafiri kwenye ‘bodaboda’.

Video iliyokuwa gumzo ndani ya muda mchache ambayo awali iliwekwa kwenye Facebook, imemuonesha mwanamke ambaye amevalia nguo zinazoacha sehemu kubwa ya mwili wake akiwa amepakiwa na mwanaume mmoja kwenye pikipiki, akijinyoa vinyweleo vya miguu na mapaja yake katikati ya jiji.

Mwanamke huyo ambaye jina lake halijafahamika, anaonekana akipiga sehemu mbalimbali za pikipiki hiyo kuondoa uchafu kwenye wembe anaoutumia.

“Ama kweli, inaonekana leo chumvi ya maji ya bahari itapenya vyema kwenye ngozi ya mwanamke huyu,” aliandika mtumiaji mmoja wa Facebook akiamini kwa mavazi yale wawili hao walikuwa wakielekea fukwe za jiji la Miami.

Aidha, wanaharakati wa masuala ya usalama barabarani wamekosoa vikali video hiyo wakidai kuwa inaonesha uzembe wa hali ya juu kwani abiria na dereva wote hawajavaa kofia ngumu (helmet) kinyume cha sheria.

Wengi wanauliza inawezekanaje katikati ya mitaa ya Florida mtu akakatiza akiwa anavunja sheria hadharani kwa kuendesha bila kuwa na kofia ngumu huku abiria naye akifanya yale aliyopaswa kuyafanya akiwa ametulia, bila kutiwa nguvuni na vyombo vya dola.


Bila shaka, video hiyo ingekuwa imechukuliwa hapa Tanzania, yangetokea kama yale ya yule dereva wa basi mwenye mbwembwe aliyeachia usukani akicheza ‘Muziki’ ya Darasa na Ben Pol. Kwa ufupi angesukumwa ndani.

Wizara ya Afya yatoa msaada wa Kisaikolojia mkoani Njombe
Serikali kujenga mazingira wezeshi katika sekta ya kilimo

Comments

comments