Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua mafunzo kwa wavuvi yenye lengo la kuzifahamu zana za uvuvi zinazoruhusiwa kwa mujibu wa sheria na kutambua fursa zilizopo katika sekta ya uvuvi hali itakayoleta tija kwa maisha yao na ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Akizindua mafunzo hayo Kitaifa kwa wavuvi katika mwalo wa Kilindoni, Wilaya ya Mafia mkoani Pwani, Waziri Mpina amesema kufuatia wavuvi wengi na sekta ya uvuvi kwa ujumla kukumbwa na changamoto nyingi ndio iliyoisukuma wizara yake kuanzisha mafunzo hayo ili kujenga uelewa wa pamoja na kuondoa kasoro zilizopo.

Amesema licha ya Tanzania kuwa na eneo kubwa la uvuvi katika kipindi cha mwaka 2016/ 2017 Tanzania ilitumia jumla ya sh. bilioni 56 ambapo mwaka 2017/ 2018 imefikia sh Bilioni 150 kwa ajili ya kuagiza samaki kutoka nje ya nchi fursa ambayo ingetumiwa na wavuvi wa Tanzania kukuza uchumi wao.

Video: Aliyekuwa naibu katibu mkuu BAVICHA ahamia CCM
Watu 3 wafariki, 150 hawajulikani walipo baada ya boti kuzama