Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameteketeza tani 11 za samaki aina ya Sato wenye viambata vya sumu waliongizwa nchini kutokea nchini China bila ya kuwa na nyaraka zozote halali zinazowaruhusu kuingiza mzigo huo nchini.

Samaki hao wanakadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 66 ambapo mmiliki wake aliwasilisha nyaraka zikionesha amenunua samaki kutoka kwenye mnada ulioendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kontena hilo kutelekezwa na kukosekana mwenyewe katika Bandari ya Dar es Salaam.

Nikki Mbishi aelezea ujumbe ‘tata’ aliopewa na Ruge
Tanzania na Brazil zaingia makubaliano ya kuinua kilimo cha Pamba nchini

Comments

comments