Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wanaoshiriki kozi fupi ya tano ya viongozi wahakikishe watakaporudi kwenye maeneo yao ya utendaji wawe wamebadilika kimtazamo, kihoja, kiushauri pamoja na utoaji maamuzi.

Majaliwa amesema hayo wakati akifungua kozi ya tano ya muda mfupi ya viongozi inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Amesema chuo hicho kilianzishwa kwa lengo la kulisaidia Taifa kujenga uwezo wa viongozi ili wanaohitimu mafunzo hayo wawe na uchambuzi wa kina na wa kimkakati ili kuweza kutatua mambo mbalimbali ya usalama wa Taifa na matatizo yanayotakiwa kushughulikiwa kimkakati.

“Chuo hiki kilianzishwa ili kuwaleta washiriki kutoka taasisi zote za Serikali na sekta binafsi waweze kujadili mambo mbalimbali ya kimkakati ili wanapokuwa wanatekeleza wajibu wao watambue kuwa ni kwa kiasi gani matokeo ya maamuzi yao yataathiri mambo ya kijamii, kiuchumi, uhusiano wa kidiplomasia na siasa za ndani kwa ujumla wake”.

 

TCU yatoa saa chache kufunga dirisha la maombi elimu ya juu
Video: kazi niliyotumwa ni hii, hayo ndiyo mambo natakiwa nifanye – Jerry Muro

VIDEO: Zitto avaana na Nape…, Chadema yaja na uamuzi mgumu

Willian afichua siri ya kilichotaka kumuhamisha Chelsea
Wachezaji wamtetea Unai Emery