Uongozi wa Dar24 Media unawashukuru sana wote wanaoendelea kutoa michango yao kwa ajili ya kuokoa maisha ya mtoto Mariam Mwema Ibrahim (16), ambaye tayari yupo nchini India kwa ajili ya matibabu.

Dar24 pia inatoa shukrani kwa makampuni mbali mbali ambayo yanaendelea kujitoa kwa dhati kumsaidia Mariam kupitia kampeni yake ya Tuko Pamoja ambayo ni endelevu na inalenga kuwasaidia watoto wenye matatizo mbali mbali ya kiafya.

Makampuni hayo ni DataVision Internationa, MacLeans BeneCIBO, Amifan, OnDemand na M-Lipa.

Mariam amesafirishwa kwenda India kwa ajili ya matibabu kufuatia ugonjwa wa tumbo unaomsumbua unaofahamika kitaalam kama ‘Intestinal Obstruction’ ambao umepelekea Mariam kufanyiwa operesheni 10 bila nafuu.

Kutokana na ugonjwa huo Mariam hawezi kula maisha yake yamejaa maumivu makali muda wote, si usiku wala mchana. 

Bado Tuko Pamoja inaendelea kupokea michango yako mtanzania kwani bado gharama za matibabu hazijatimia hivyo mchango wako utasaidia sana kuokoa maisha ya mtoto Mariam kwa kuendelea na matibabu nchini India.

Mimi na wewe ni sehemu kubwa sana ya furaha tena kwa Mariam anayesumbuliwa na Intestinal Obstruction. Mariam anahitaji kwa dhati kabisa msaada wako ili akapate matibabu nchini India, gharama ya matibabu ni zaidi ya shilingi milioni 44 za kitanzania. Tuma Mchango wako sasa kupitia Tigo Pesa, M Pesa, Airtel Money. Namba ya Kamupuni 400700, Namba ya kumbukumbu 400700. TUKO PAMOJA #OkoaMaishaYaMariamTusikubali kumpoteza Mariam

Kwa mawasiliano zaidi tupigie kupitia: 0679 979 786 au +255 222 701 845/6
Email: info@dar24.com

Shein atoa msamaha kwa wafungwa 12
Amchoma visu mpenzi wake akidai ‘Mungu’ amemtuma