Wakili na Mwanasheria Msomi wa Kujitegemea, Leonard Manyama amemtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad kujiuzulu baada ya kutofautiana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa Prof. Assad anapaswa kujiuzulu ili aweze kulinda heshima yake kwani muda wake wa utumishi umebaki mfupi.

Amesema kuwa kitendo cha kukataliwa kufanyakazi na bunge kinamfanya apoteze sifa ya kuendelea kuwa katika nafasi hiyo ya CAG, hivyo anapaswa ajitathimini mara mbili kabla ya uamuzi mwingine kuchukuliwa.

”Unajua CAG, Prof. Mussa Assad anatakiwa ajitafakari, namaanisha ajiuzulu, kitendo cha kukataliwa kufanyakazi na bunge ni kigezo tosha cha kumfanya achukue maamuzi, hapa maana yake tayari ameshapoteza sifa ya kuendelea na nafasi hiyo,”amesema Wakili Manyama

Hata hivyo, siku za hivi karibuni, kamati ya maadili ya bunge ilimkuta na hatia kiongozi huyo mara baada ya kutumia maneno kwamba bunge la Tanzania ni dhaifu alipokuwa akizungumza na kituo kimoja cha redio cha kimataifa.

  • LIVE: Yanayojiri katika ziara ya Rais Magufuli mkoani Mtwara
  • LIVE: Yanayojiri katika ziara ya Rais Magufuli Mkoani Ruvuma
  • JPM amfagilia Mkapa, ‘bila yeye nisingekuwa waziri au Rais
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Aprili 6, 2019
Aliyewatapeli mahujaji mwaka 2017 anusurika kichapo

Comments

comments