Wakili wa kujitegemea, Leonard Manyama ametoa ufafanuzi kuhusu sakata la kuvuliwa ubunge kwa aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Amesema kuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai alikuwa sahihi kuchukua uamuzi huo kwani vifungu na taratibu za bunge hazikufuatwa na chama chake.

”Ni lazima tujiulize, Tundu Lissu alikuwa Ulaya kwaajili ya matibabu au alikwenda kufanya mahojiano na vyombo vya habari vikubwa kuichafua nchi na kufanya midahalo ya kutukana viongozi wakuu wa nchi,”amehoji wakili Manyama

Aidha, Manyama amewataka wabunge kuelewa maharti ya Ibara ya 70 na 71 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, ambayo inasema usipohudhuria vikao vitatu pasipo na ruhusa ya spika, utakuwa umejivua ubunge.

Hata hivyo, siku kadhaa zilizopita, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai alitangaza kuwa, jimbo la Singida Mashariki liko wazi hivyo alishaijulisha tume ya uchaguzi ilikuendelea na utaratibu wa uchaguzi.

Kocha wa Senegal awapigia saluti Uganda
Video: Kenyatta amkosha Magufuli, 'Umekuwa Rais wa kwanza kuja Chato'