Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewapiga marufuku viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kuwanyang’anya bidhaa wafanyabiashara wadogo na badala yake amewaagiza viongozi wote nchini kujielekeza katika kutatua kero zinazowakabili wananchi.

Ametoa agizo hilo alipokuwa anasalimiana na wananchi waliokusanyika mjini Sengerema akiwa njiani kuelekea Chato Mkoani Geita kwa mapumziko.

“Nilishasema viongozi wote niliowateua mimi msisherehekee uteuzi, mtasherehekea siku mkimaliza uongozi, nataka mchape kazi, tatueni kero za wananchi na waleteeni maendeleo,”amesema JPM

Aidha, Dkt. Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kufuatilia na kutatua kero zinazowakabili wafanyabiashara hao.

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa juhudi za kujenga Tanzania mpya zinakwenda vizuri kutokana na mafanikio makubwa yaliyoanza kupatikana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na utatuzi wa kero za wananchi.

Mexico yateketeza tani 50 za dawa za kulevya
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 19, 2018