Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa atawasaka popote pale walipo, watu wote waliotelekeza watoto bila kujali vyeo vyao.

Ameyasema hayo hii leo jijini humo alipokuwa akiwasikiliza akina mama waliotelekezwa na waume zao, ambapo amesema kitendo hicho ni cha kikatili.

Amesema watu hao watasakwa popote pale walipo, hivyo ni vyema wakajisalimisha wenyewe kabla sheria haijachukua mkondo wake.

“Mtu yeyote aliyekupa mimba, awe ni mwalimu, mwanasiasa, kiongozi yeyote, awe anafanyakazi benki, tutamfuata huko huko alipo,”amesema Makonda

Ndugai awashukuru wabunge, awaombea wasipitie machungu aliyoyapitia
Eusebio Di Francesco aapa kuifunga FC Barcelona