Urusi imefanya majaribio ya kombora lake jipya la nyuklia linaloitwa intercontinental ballistic missile (ICBM) linaloweza kufika sehemu zote za dunia, kwa mujibu wa Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo.

Waziri huyo aliyeweka video ya tukio hilo kwenye twitter amesema kuwa jaribio hilo limefanyika Ijumaa iliyopita. Ameongeza kuwa kombora hilo linachukua nafasi ya kombora la kisovieti liitwalo Veovoda.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin alifichua kwa mara ya kwanza maelezo ya kombora hilo mwezi Machi. Akihutubia taifa hilo, alisema ICBM inaweza kupiga eneo na kona yoyote ya dunia.

Urusi imeendelea kujiimarisha kijeshi huku ikiwa inauhusika katika migongano ya kijeshi ya mataifa mbalimbali, ikiwatetea washirika wake kama Syria.

Majaribio ya makombo ya nyuklia ya aina hiyo yalikuwa yakifanywa pia na Korea Kaskazini, hatua iliyozua mgogoro na Marekani pamoja na washirika wake.

Mbivu na mbichi za Michael Wambura kujulikana kesho
Meya wa jiji atekwa nyumbani kwake