Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa Kama Rais Magufuli akimteua kuwa kiongozi hatakubali bila kufanyika kwa mashaurino ya ndani ya chama na kama chama kikiona jambo hilo halina maslahi ya Chama atakataa uteuzi huo.
Zitto amesema anachokifanya Rais Magufuli kwa sasa na tamaduni mpya, kwani zamani waliteuliwa viongozi wa upinzani kuwa wabunge na sio nafasi za kisiasa kama alivyoteuliwa aliyekuwa mwenyekiti wa ACT, Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumzia kuhusu kuvuliwa uwenyekiti, Anna Mghwira, Zitto amesema imekuwa changamoto kubwa kwao kwani nafasi ya ukuu wa Mkoa ni nafasi ya kisiasa tofauti na kama angeteuliwa kuwa Mbunge kama ilivyozoeleka hapo awali katika teuzi mbali mbali.

Aidha, Rais Magufuli wakati akimuapisha Mkuu mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa kamwe katika teuzi zake hatateuwa Mbunge kutoka upinzani.

 

Magazeti ya Tanzania leo Juni 10, 2017
Video: Mghwira apinga ACT, Ni Bonge la Bajeti