Msanii wa Hiphop nchini Marekani, Micheal Ray Stevenson maarufu kama Tyga anaetamba na wimbo wa ‘Girl have fun’ ametolewa katika sherehe ya kuzaliwa ya mcheza masumbwi, Floyd  Mayweather Jr iliytofanyika Califonia nchini Marekani.

Tyga aliingia katika mtifuanao mkali na moja kati ya waalikwa ambaye bado haijafahamika kama wanabifu.

Hali hiyo imepelekea msanii huyo kutolewa nje ya ukumbi na walinzi. Kwa mujibu wa ripoti ya TMZ, Tyga alivyofika nje alionekana bado anahasira na kutaka kuinyakua bastora ya mlinzi wake lakini watu waliokuwa karibu walifanikiwa kumdhibiti ili kumnusuru na kesi ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Hata hivyo ilichukua muda hadi rapper huyo wa ‘Taste’ kutulia lakini baadaye alitulia na aliamua kuondoka eneo hilo.

Mchungaji 'afufua maiti' akioneshwa Live kwenye TV, maswali yazidi majibu
Mahakama yatoa uamuzi hati ya kumkamata Lissu, yawaonya wadhamini

Comments

comments