Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye amesema kuwa kazi yao kubwa ni kuangalia changamoto zipi zinazokwamisha uwekezaji na kuziwasilisha serikalini kwa ajili ya kutunga sera zitakazosaidia kufungua fursa kwa wawekezaji.

Amesema kuwa kazi kubwa ni kuifanya sekta binafsi kuiona fursa na nafasi ya kuiona pesa inapatikana sehemu gani ambayo ni sahihi kwa ajili ya uwekezaji.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kwasasa wanashirikiana na serikali katika kuondoa vikwazo na changamoto ambazo zimekuwa zikisababisha usumbufu.

Aidha, akizungumzia Utawala wa Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa umeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kwani Rais anapambana na suala la rushwa ambalo lilikuwa tatizo sugu.

Mpina awatumbua watumishi 91
Video: Dkt. Ndugulile asema huduma za afya zimeaimarika