Wakala wa Majengo nchini Tanzania (TBA) imeandaa utaratibu mzuri wa kufanya malipo kwa wateja wake ambao utakuwa rahisi popote pale walipo.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mshauri Mwendelezaji Miliki kutoka TBA, Shauri Ramadhani alipokuwa akizungumza na Dar24Media kwenye maonyesho ya biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba.

Amesema kuwa kwasasa kuna mifumo minne ambayo itamrahisishia mteja au mtumishi kufanya malipo popote pale alipo, hivyo kuondokana na changamoto zilizokuwepo hapo awali.

”Kwakweli kwasasa mteja wetu au mtumishi anaweza kufanya malipo kwa njia nne ambapo atakuwa na uhuru wa kuchagua atumie njia ipi ambayo ni rahisi kwake,”amesema Ramadhani

Aidha, Ramadhani amewahamasisha wananchi na wadau mbalimbali kutembelea banda la TBA lililopo katika viwanja vya Sabasaba ili waweze kujifunza mambo mbalimbali yanayohu Wakala wa Majengo Tanzania.

TFF yamfungashia virago Amunike
Nyongo awatahadharisha watoroshaji wa Madini