Kama bado ulikuwa bado hujatazama wimbo wa baba yake Diamond Platinumz, nimekuwekea hapa chini.

Aidha mzee Naseeb amefunguka na kudai kuwa ameamua kufanya nyimbo hiyo kwa lengo la kutaka kuwasaidia wasanii hao wadogo waliomuomba kufanya nae kazi hiyo kwa muda mrefu inayoenda kwa jina la Mwewe kama njia rahisi itayowasaidia kutoka na kufahamika zaidi kimuziki.

Ndiyo, wimbo huo umefanya vizuri sana hasa kipande ambacho Mzee Abdul ameimba kwani watu mbalimbali wameshare kupitia mitandao ya kijamii na umepata umaarufu mkubwa.

Mzee Abdul alikubali kufanya kazi nao akiwa na malengo ipo siku kupitia wimbo huo atapata fedha zitazomsaidia kufanya matibabu ya miguu yake ambayo inamsumbua, kama ambavyo ameonekana kwenye video hiyo hakuweza kusogea kutoka eneo moja kwenda jingine hata wakati anacheza, amecheza akiwa amesimama eneo moja kutokana na tatizo lake la miguu.

Pia amemshukuru, Diamond, Queen Darlin na Bi Sandra kwa kuukubali wimbo huo na anaamini ipo siku ataweza kufanya kolabo nao.

Tazama hapa.

Wahamiaji 12 wakamatwa mkoani Njombe
Video: Ziara ya Rais Magufuli mkoani Ruvuma - Namtumbo

Comments

comments