Mkali wa muziki wa miondoko ya ‘Afropop’ kutoka Nigeria, David Adedeji Adeleke maarufu kama Davido ameachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Assurance’.

Davido ameachia video ya wimbo huo ikiwa ni siku chache baada ya kufanya show kali katika tamasha la  Castle Lite Unlocks lililofanyika jijini Lagos Nigeria sambamba na msanii J Cole kutoka Marekani.

Wimbo huo unasemekana kuwa ni zawadi kwa mpenzi wa muda mrefu wa Davido anayeitwa Chioma ambaye mbali na kumuimbia wimbo huo amemnunulia gari aina ya Porsche.

Itazame video hiyo hapa chini;

Makombora mengine yashushwa Syria, Israel yatamba
Steve Nyerere ataka wasanii kumiliki bima, ''tutakuwa watu wa kuomba msaada''