Mwanamuziki Mkongwe na gwiji wa muziki katika miondoko ya Country, Mmarekani Kenny Rogers aliyezaliwa mwaka 1938 amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake huko Sandy Springs, Georgia, Marekani.

Familia yake imesema Rogers aliyekuwa Mwandishi wa Nyimbo, Muigizaji, Muimbaji na ‘Producer’ amefariki kwa amani (peacefully) akiwa chini ya Uangalizi wa Muuguzi huku akiwa amezungukwa na familia yake

Rogers, alitamba kwa nyimbo zake nyingi zikiwemo The Gambler, Lady, Islands in the Stream na Lucille, huku akiwa ameuza rekodi zaidi ya Milioni na kushinda tuzo 3 za Grammy.

Kama muigizaji ametokea kwenye filamu ya Six Pack mwaka 1982 na katika tamthilia kadhaa maarufu za runinga kama The Gambler franchise, Christmas in America na Coward of the County…, Bofya hapa kutazama wimbo wake wa The Gambler

Wachezaji wa kigeni wawekwa mtegoni
Daladala zapigwa marufuku kusimamisha abiria

Comments

comments