Timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, imekuwa miongoni mwa timu nne zilizofuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kuifunga Uganda  ‘The Crane’ magoli matatu kwa sifuri.

Mechi hiyo dhidi ya Taifa Stars na Uganda the Craines imechezwa katika Uwanja wa Taifa leo (Jumapili, Machi 24, 2019) ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliwaongoza Watanzania kushuhudia mechi hiyo.

Video: Goli la Kwanza la Taifa Stars Vs Uganda 1 – 0 AFCON

Taifa Stars imefuzu michuano hiyo itakayofanyika mwaka huu nchini Misri baada ya kupita miaka 39 tangu mara ya mwisho kucheza michuanohiyo.Timu hiyo kwa sasa imeungana na Burundi, Kenya na Uganda kufuzu michuano hiyo.

Magoli ya  Simon Msuva, Erasto Nyoni na Agrey Morris yalichangia kuivusha Taifa Stars, ambapoMsuva alianza kwa kuipatia gori timu ya Taifa ya Tanzania dakika ya 20 baada ya mechi hiyo kuanza, Nyoni aliipatia Taifa Stars goli la pili dakika ya 50 na dakika sita baadae Moris aliipatia timu ya Taifa goli la tatu.

Video: Goli la pili la Taifa Stars Vs Uganda 2 – 0 AFCON

Kufuatia ushindi huo wachezaji wote wa Timu ya Taifa ya Tanzania wamejihakikishia kila mmoja kuondoka na kitita cha shilingi milioni 10 kutoka kwaKamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akizungumza na wachezaji hao jana wakati Waziri Mkuu alipotembelea kambi yao, Makonda ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kamati yake itatoa sh. milioni 10 kwa kila mchezaji wa timu hiyo iwapo timu itafuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Video: Goli la tatu la Taifa Stars Vs Uganda 3 – 0 AFCON

NayeWaziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala yeye aliwaahidi kuwapeleka katika mbuga yoyote ya wanyama watakayoichagua kwa ajili ya mapumziko iwapo wachezaji hao wataibuka na ushindi katika mechi dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda.

Live: Rais Magufuli akutana na Taifa Stars Ikulu baada ya ushindi 3 - 0 dhidi ya Uganda
Video: Maalim Seif: watapata tabu sana, RC Hapi apewa siku saba