Mbunge wa mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), amewataka wanasiasa kutowatumia vibaya wasanii kwa manufaa yao binafsi.

Ameyasema hayo jana Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akisoma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Aidha, Sugu amemtaka msanii ‘Roma’ kujitokeza hadharani kusema ukweli ni kipi kilichotokea na ni nani aliyehusika katika tukio hilo la utekwaji wake na wenzie.

“Wanasiasa tunatakiwa tuwaheshimu wasanii kwani ni kioo cha jamii, kuwatumia na kuwaterekeza mtakuwa hawatendei haki,”amesema Mbilinyi.

Hata hivyo, katika hatua nyingine mbunge huyo amewataka wasanii kuungana na wanahabari katika kutetea maslahi yao pindi wanapokuwa wamekumbana na majanga.

Breaking: Wanafunzi 29, walimu 3 wapoteza maisha ajali ya basi Karatu
Video Mpya: Darassa afyatuka tena, aachia video ya ‘Hasara Roho’