Mbunge wa Mbeya mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, amejitokeza katika mapokezi ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli mkoani Mbeya.

Sugu ametambulishwa na Rais Magufuli, msafala wake ulipofika mjini Mwanjelwa, ambapo amesema kuwa maendeleo hayachagui chama ndiyo maana Mbunge huyo kupitia chama pinzani cha CHADEMA ameungana na viongozi wenzake pamoja na wananchi kumpokea

Alipo tambulishwa licha ya kutopata nafasi ya kuzungumza kwa wakati huo Sugu aliwasalimia wananchi kwa furaha huku akiwaonesha ishara ya chama chake.

Rais Magufuli ataendelea na ziara yake mkoani Mbeya kwa muda wa siku nane na atapata nafasi ya kuzungumza na wananchi kwenye maeneo mbalimbali…, Bofya hapa kutazama

Serikali yatangaza mapumziko kesho, yazima shamrashamra kuokoa milioni 988.9
LIVE: Ziara ya Rais Magufuli Mbeya baada ya kuwasili akitokea nchini Malawi

Comments

comments