Mkali wa RnB aliyetikisa miaka kadhaa iliyopita, Steve RnB ameweka wazi kuwa yeye ni moja kati ya watu wachache ambao Bongo Fleva sio aina ya muziki wanaousikiliza.

Akifunguka katika mahojiano maalum na Dar24, msanii huyo aliyekita kwenye mkondo wa muziki kwa sauti yake ndani ya ‘Tabasamu’ ya Mr. Blue, ameeleza kuwa kwa miaka kadhaa aliacha kusikiliza Bongo Fleva kwa sababu haitamuongezea kitu kwenye sanaa yake.

“Mara nyingi huwa sipendi kusikiliza kitu ambacho hakitanipa kitu. Muda mwingi nimetumia kusikiliza nyimbo za wasanii kama wa Jamaica, kwa sababu huwa kuna vitu fulani vinavyoni-inspire (vinavyonihamasisha),” Steve amefunguka.

Ameeleza kuwa tangu alipoachia ‘Jambo-Jambo’ alijikita katika kusikiliza muziki wa nje wa mahadhi ambayo anayakubali.

“Ndio maana hata kuna baadhi ya kazi ambazo unaweza kuniambia lakini majina yake nikasahau. Kwangu mimi nimekuwa inspired (nimehamasishwa) sana na muziki wa Jamaica,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Steve alifunguka kuhusu nani anayepaswa kupewa taji la Ufalme wa RnB kwa sasa kwa kuzingatia ushindani uliopo.

Angalia video hapa chini kupata kwa undani alivyofunguka, nani anapaswa kuwa Mfalme, kuhusu maisha ya uhusiano na mengine mengi. Je, anawatambua vipi Jux, Ben Pol na wengine?

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 11, 2019
Pacquiao aeleza kwanini Mjapan alilia baada ya kupigwa na Mayweather

Comments

comments