Mchekeshaji Steve Nyerere ametangaza fursa kwa kila Mtanzania mwenye kipaji cha kuigiza kujitokeza kwenye usaili utakaolenga kutafuta waigizaji watakaoshiriki kwenye tamthilia inayotarajiwa kuanza kuandaliwa Septemba mwaka huu, itakayoshirikisha ‘mastaa’  wa hapa nchini na nyota wachanga watakaopatikana katika usaili huo.

Steve amesema usaili huo utafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 10 mwezi huu kuanzia saa tatu asubuhi. Amesema wahusika ni waigizaji wote wachanga na hakutakuwa na masharti yoyote. Hivyo, amewaomba watu kujitokeza kwa wingi ili kutimiza ndoto zao kupitia kiwanda cha filamu.

Usaili unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Muigizaji huyo amewaomba wazazi wenye watoto wenye vipaji vya kuigiza wawapeleke watoto wao ili waweze kupata fursa hiyo.

Aidha, amesema tamthilia hiyo itakuja kama muundo wa tamthilia ya Isidingo, ambayo ni moja ya tamthilia yenye misimu (Seasons) mingi zaidi ambapo hadi kufikia Novemba 21, 2018 takwimu zinaonyesha imekuwa na sehemu (episodes) 5080 na misimu 21.

Tamthilia hiyo iliyochezwa na watu kutoka Afrika Kusini kwa mara ya kwanza ilianza kuonyeshwa Julai 7, 1998 hadi leo ikiwa bado inaendelea kuonyeshwa na kutazamwa na baadhi ya wapenzi wake.

Sikiliza video yote hapa chini kuona jinsi alivyoielezea tamthilia yake akiifananisha na ‘Isidingo’.

‘Yesu feki’ wa Kenya hajafa, aonekana tena mitaani, afunguka
Mifuko mbadala yawaponza maafisa TBS, watumbuliwa