Siku kama ya leo mwaka 1996, ni tarehe yenye rangi nyekundu kwenye kalenda ya mioyo ya watu wengi.

Ikiwa ni Mei 21, siku ya kumbukizi ya miaka 23 ya tukio la majonzi na simanzi lililoikumba Tanzania na Dunia kwa ujumla, Dar24 Media tumekuandlia makala kuhusu tukio hilo ambalo lilitokea siku ya Jumanne.

Siku hiyo rangi ya maji ya Ziwa Victoria iliyozoeleka kuwa ile iliyoakisi uzuri wa rangi ya mawingu, siku hiyo ilifyonza wekundu wa damu ya Watanzania na raia wa nchi nyingine, zaidi ya 894 waliopoteza maisha baada ya meli ya MV Bukoba kuzama ndani ya ziwa hilo.

Tazama hapa

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 22, 2019
Video: Hii ndiyo adhabu utakayopata ukikutwa na mfuko wa plastiki

Comments

comments