Msanii kutoka WCB Harmonize anayetamba na wimbo wake wa My Boo aliomshirikisha mkongwe wa muziki wa bongo fleva Q Chief amesema kuwa ‘hajamsaini’ msanii huyo bali amemsaidia gari aina ya Porte kwaajili ya usafiri ambao utamsaidia katika kazi zake za muziki.

Harmonize ambaye ametoa mfululizo wa nyimbo zake yaani EP siku ya jana akiwa amemshirikisha Q Chief, amesema kuwa tatizo la Q Chief ni la kijamii hivyo hatakiwi kuachwa peke yake kwani ni msanii ambaye alikuwa anaushawishi  kwa vijana wengi kuingia katika muziki na kuna ambao tayari wamepata matunda ya sanaa ya muziki.

Aidha, amesema kuwa, mkongwe huyo wa muziki wa bongo fleva atakuwepo katika tamasha la wasafi festival ambapo watatumbuiza nyimbo alizomshirikisha katika mfululizo wa nyimbo ‘EP’ katika jukwaa la wasafi festival.

Kamanda Muroto awatahadharisha matapeli jijini Dodoma
Video: "Sitegemei kukwama kama wengine" - Barnaba

Comments

comments