Serikali kupitia wizara ya kilimo imeweka bayana wakulima wa mazao ya msingi ambao wataanza katika zoezi la kusajili wakulima nchini ili kukabiliana na changamoto zao kwa urahisi.

Naibu waziri wa kilimo Omary Mgumba amesema kuwa wakulima wote wanaolima mazao yaliyo na bodi za mazao watakuwa wa kwanza kusajiliwa.

Aidha ametoa wito kwa vijana kujiajiri kwenye sekta ya kilimo kwa kutumia elimu waliyonayo kwani ajira kwenye kilimo inafursa nyingi kama, kutafuta masoko kwa kutumia mitandao, kusambaza pembejeo na kutengeneza ajira kwa watu wengine.

Video: Wachoraji Dodoma Tunaimani TACIP itatuokoa, ''Changamoto ya Rangi na Brashi''
Video: Huyu ndiye Mbunge aliye changia Miradi ya jamii kwa Nguvu zake