Halmashauri ya manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera imeadhimisha Wiki ya Elimu ya Watu Wazima yenye kauli mbiu “Elimu haina Mwisho’ wakati ambapo jamii asilimia kubwa bado ina fikra potofu juu ya dhana ya Elimu hii.

Akizungumza Mara baada ya Kuhitimisha sherehe za Maadhimisho hayo Katibu tawala wilaya ya Bukoba, Kadole Kilugala amekiri kuwepo Kwa upotoshaji wa dhana nzima ya elimu ya watu wazima, na kueleza kuwa  kuwa wengi hudhani elimu hii inalenga wazee tu au watu wenye umri zaidi ya miaka 18, jambo ambalo sio sahihi kwani Elimu hii Kwa sasa inamgusa mtu yeyote aliyekosa Elimu na stadi za maisha kubwa ikiwa ni kujua kusoma, kuhesabu na kuandika maarufu kama “K” tatu, Kwa utaratibu MEMKWA na MESKWA.

Kadole amesema takwimu zinaonesha kuwa Sensa iliyofanyika mwaka 2012 inaonesha kuwa asilimia 22 ya Watanzania hawajui kusoma na kuandika, hivyo Serikali tayari imeanza utaratibu wa kuwezesha programu hii kupitia mpango wa Elimu bila malipo na Kwa mara ya kwanza mwaka huu Manispaa ya Bukoba wametenga Milioni Nne kuongeza ufanisi wa Elimu hii…, Bofya hapa  kutazama

Siku ya kichaa cha mbwa: Watoto ndiyo waathirika wakubwa
DC Kilolo abadili madereva 10 kwa miaka minne