Nyota wa Hollywood, Arnold Schwarzenegger ameshambuliwa kwa teke nchini Afrika Kusini katika hafla na mashabiki wake.

Schwarzenegger ambaye pia alikuwa Gavana wa jimbo la California mwenye umri wa miaka 71, alikuwa anapiga picha na mashabiki wake katika mji wa Johannesburg na mashabiki wake wakati wa mashindano ya kuruka kamba katika hafla yake ya michezo barani Afrika

Wakati tukio hilo likiendelea mtu huyo alipomshambulia kwa teke kutoka nyuma yake, na nyota huyo wa ‘The Terminator’ alionekana akikaribia kuanguka baada ya teke hilo, huku mshambuliaji wake akianguka chini kisha kukamatwa kwa walinzi na kabidhiwa maafisa wa Polisi kulingana na maafisa wa hafla hiyo.

 

 

Mbowe afunguka sababu za Lowassa kuikimbia Chadema
Wanaume tereza Kigoma wazua gumzo, LHRC yawakomalia

Comments

comments