Kufuatia kifo cha aliyekuwa mpendezesha video, Agness Gerald Waya maarufu kama Masogange aliyefariki dunia April 20, 2018 siku ya ijumaa, Ibada ya msiba huo imewakuwakutanisha wasanii wa bongo fleva, Ali kiba na Diamond Platinumz katika viwanja vya Leaders Club.

Ambapo wasanii hao walipata nafasi ya kutoa salamu za mwisho kwa ndugu jamaa na marafiki wa karibu wa marehemu na kutumia nafasi hiyo kuwatia moyo na kuwakumbusha kuwa msiba huu ni wa wetu sote na kuonesha jinsi gani wameguswa na kifo cha Masogange.

Wasanii hao wamekumbusha jamii kuishi kwa sala na kuishi tukifahamu kuwa sisi sote wa Mungu hivyo tutumie muda mwingi kufanya ibada na kutenda matendo mema kwani hatujui saa wala dakika ya mwisho ya pumzi yetu.

Ibada hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo ndugu jamaa na marafiki na wasanii wa bongo akiwemo Harmonize, Chege, Shilole, Dogo Janja na wengine wengi huku wasanii wa Filamu akiwemo, Irene Uwoya, Dr. Cheni, Chopa Mchopanga na baadhi ya Viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi.

Bonyeza kitufe hapo chini kusikiliza hotuba ya Diamond Platinumz na Ali kiba katika viwanja vya Leaders Club, msibani kwa Agness Gerald Waya maarufu kama Masogange.

Magaidi washambulia kituo cha kuandikisha wapiga kura
JPM atuma salamu za pole kwa familia ya Masogange