Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemsaidia Mama Mjane, Benadetha Rwendela aliyekuwa kadhulumiwa Nyumba yake Plot No. 239 Block B Kunduchi Beach kwa kupigwa Mnada na Madalali kutoka Kampuni ya Nkanya Ltd kinyume na taratibu kisha kuamriwa kuondoka ndani ya siku 30.

Baada ya Makonda kuona taarifa hizo kwenye baadhi ya Vyombo vya Habari na Mitandao alimwita Mjane huyo Ofisini kwake kisha kumkutanisha na Wanasheria wa Mkoa na kubaini utapeli mkubwa uliotumika kuuza
Nyumba hiyo kutokana na watu kufoji nyaraka ikiwemo Sahihi ya Mwenyekiti wa Mtaa huku nyumba hiyo ikiwa na Zuio la Mahakama.

Aidha imebainika Kuwa Hati za Nyumba hiyo zilifojiwa kisha kutumika kuchukuwa Mkopo wa Shilingi Billion Moja pasipo mmiliki wa nyumba kujua kinachoendelea.

Kwa upande wake Mjane huyo Bi. Benadetha Rwendela ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwajali Wananchi wake na kuwasaidia pale wanapopata matatizo huku akimpongeza Rais Magufuli kwa kumteua RC Makonda.

Kamati ya nidhamu yamfungia Obrey Chirwa
Video: Namshangaa Mbowe kumkana Lowassa- Cyprian