Mkongwe wa muziki wa Hip hop Joseph Haule maarufu kama Professor Jay akiwa  kwenye mahojiano na Dar24 amesema kuwa hauelewi ugomvi wa Alikiba na Diamond, kutokana na wao kutokuwa wawazi pindi wanapowauliza ili kutatua tatizo lilipo baina yao.

Amesema kuwa wasanii hao ndio waliofanikiwa kuitambulisha vizuri tasnia ya muziki wa bongo fleva nje ya Nchi na kufanikiwa kuingia kwenye tuzo mbalimbali duniani.

“Kila nikiwauliza kuna tatizo gani wote wanasema hakuna tatizo inakuwa ngumu kuwapatanisha wao ni icon katika muziki hakuna haja ya bifu” alisema Professor Jay

Katika hata nyingine Msanii huyo ambaye siku ya jana alitumbuiza katika jukwaa la wasafi festival amempongeza Diamond kwa kukutanisha wasanii wa zamani na wasanii wasasa katika jukwaa moja,…Bofya hapa kutazama zaidi

Waliokuwa makocha wa Simba watajwa kutua KMC
DC Mjema ashiriki kumtafuta aliyezama mto Msimbazi

Comments

comments