Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole ametaja sababu za chama hicho kushinda uchaguzi jimbo la Monduli ni kuwa chama kilikuja na mkakati  wa  kupeleka miradi ya maendeleo pamoja na kuwakopesha wananchi wanyama aina ya Mbuzi.

Polepole amesema hayo leo Septemba 18, 2018 jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa chama hicho kimeshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Monduli na Ukonga kwa kunadi sera za maendeleo ya miaka 5.

“Tuliwakopesha Mbuzi wakulima hasa wakina mama na familia masikini, tuliwakopesha Mbuzi na walilipa Mbuzi Kalanga akiwa upinzani, lengo lilikuwa ni kuwawezesha wananchi wa Monduli kiuchumi.” amesema Polepole

Aidha, amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda hakupaswa kufanya sherehe ya kulipongeza jeshi la Polisi kwa kile alichokidai waliyafumbia macho baadhi ya matukio ya uvunjaji wa amani.

Hata hivyo, katika uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika septemba 16 mwaka huu CCM ilibuka kidedea katika Jimbo la Ukonga ambapo walimsimamisha, Mwita Waitara kuwa mgombea na kwa upande Monduli chama hicho kilishinda kupitia mgombea wake Julius Kalanga.

 

 

 

 

Video: Waziri Mhagama atoa agizo kwa taasisi za umma na binafsi nchini, awapongeza WCF
Chadema kula sahani moja na mawaziri walioshiriki kupiga kampeni

Comments

comments