Kinywaji maarufu cha Pombe kinachojulikana kama Kweichow Moutai kinachotengenezwa nchini China, kimezinduliwa nchini Tanzania kwa mara ya kwanza katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi huo alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda ambapo pia ulienda sambamba na maonyesho ya utamaduni na utalii wa China kupitia mkakati wa kukuza masoko na ushirikiano baina ya nchi hiyo na nchi za nje ikiwemo bara la Afrika ujulikanao kama ‘The Belt and Road Initiative’.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wageni mbalimbali ikiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela, Wanadiplomasia, Viongozi wa Serikali, Maofisa Waandamizi wa Serikali na wawakilishi wa makampuni ya biashara na taasisi za kukuza utamaduni wa China na Tanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mkuu Msaafu, Mizengo Pinda, alipongeza jitihada zinazofanywa na China kuwekeza na kufanya biashara barani Afrika, ikiwemo kusimamia miradi mikubwa ya ujenzi.

Kwa upande wake Mjumbe wa bodi na Naibu Katibu wa Bodi ya Moutai, Wang Yan amesema kuwa miaka 40 iliyopita nchi ya China ilikuwa miongoni mwa mataifa maskini duniani kuliko umaskini uliopo katika baadhi ya nchi za Afrika.

“Kama Moutai, tumechagua Afrika kutokana na kuwa na ushirikiano mzuri katika kipindi kizuri kilichopita na ushirikiano huu unaonekana utazidi kuimarika katika siku zijazo na kuongeza mafanikio,” amesema Wang Yan

Serikali yatoa wito kwa wadau kukarabati kituo cha kitalii
Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa yateketeza Nyavu na Mitumbwi Bandia