Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa bajeti ya serikali kuu inahitaji nidhamu ya hali ya juu katika matumizi yake.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa katika matumizi ni lazima fungu lijulikane ndipo matumizi yaanze.

”Ni lazima hapa tuiangalie kwa makini bajeti hii,na matumizi ya bajeti yalenge katika sehemu husika ili kuweza kutatua changamoto na matatizo mbalimbali,”amesema Prof. Lipumba

Amesema kuwa matumizi yagawiwe kulingana na sera ya serikali ili kuweza kujenga mazingira mazuri ya utekelezaji mzuri wa bajeti iliyopitishwa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa jambo linaloathiri utekelezaji wa bajeti ni uanzishaji wa sera na utamkaji wa ahadi katika majukwaa ya kisiasa ambayo hayaendani na vipaumbele vilivyotumiwa kuandaa bajeti.

Mke wa waziri mkuu atozwa faini
Wakulima wilayani Mbulu waiomba serikali kupeleka wataalamu wa kilimo