Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga wanaendelea kuwakosa nyota wao muhimu kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Mwadui FC,

Hayo yamesemwa na msemaji wa timu hiyo,  Dismas Ten alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa wachezaji watakao kosekana katika mchezo huo ni Donald Ngoma, Geofrey Mwashiuya, Thabaan Kamusoko na Obrey Chirwa.

“Tunawachezaji wetu ambao bado ni wagonjwa na wataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Mwadui huku Chirwa atakosekana kwasababu anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu aliyopewa na kamati ya maadili ya TFF,” amesema Ten.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 17, 2018
Bei elekezi mpya kuwafaidisha wauza mbolea Rukwa