Mwanamuziki maarufu nchini Marekani Cornell Iral Haynes anaejulikana kama Nelly aliyetamba na wimbo wa Dillema amesimamisha show yake kwa muda baada ya kufunguliwa kamba za viatu na shabiki wake wakati akitumbuiza katika club ya Drai’s Beach  mjini Las Vegas Marekani.

Kwa mujibu wa TMZ Nelly aliamua kugeuza kibao kwa mashabiki zake na kuikatisha show  kwa muda mchache.

Aidha staa huyo alisikika akisema “Babygirl, naukubali upendo wako lakini kwanini unifungue viatu? Hapana hapana, huwezi kunifungua viatu, kama unataka kunitega sasa hilo ni jambo lingine, Imenilazimu kusimamisha na kufunga upya”.

Hata hivyo Nelly alisisitiza kuwa haihitaji mtu kumfungua kamba za viatu vyake ikiwa tayari ni mtu mzima na mashabiki hawahitaji kuwa na uhuru wa kiasi hicho alisema Nelly

Iran yailaumu Marekani kwa kuchochea mvutano
Ndugai azungumzia ukaguzi ofisi ya CAG, 'hapa hakuna atakayekwepa'

Comments

comments