Ndege aina ya Air Force one ndiyo ndege pekee inayotumika kumbeba Rais wa Marekani, ndege hiyo inatumika katika ziara zote za marais wa nchi hiyo.

Ndege hiyo inatajwa kuwa na urefu mithili ya ghorofa sita au saba huku upana ukiwa ni sawa na ndege mbili za kawaida.

Ndani ya ndege hiyo kuna kila kitu ambacho ungeweza kukiona ndani ya nyumba au ofisi ya kifahari, kuna hoteli kubwa ya kifahari kwa ajili ya chakula na vinywaji, kuna ofisi maalumu kwa ajili ya rais.

Ndani ya ofisi hiyo ya kifahari kuna mitambo maalumu inayomuwezesha rais kuongoza nchi yake au kutoa taarifa yeyote.

Pia ndege hiyo unaambiwa haipitishi risasi ni ndege ya kivita yenye uwezo wa kufanya mashambulizi ya kivita na ni ndege mojawapo yenye kasi zaidi hapa duniani.

Itazame hapa chini.

Baada ya Vanessa Mdee, ni zamu ya Nandy
Video: Hizi ndiyo silaha zilizotumika kumteka Mo Dewji

Comments

comments