Mkurugenzi Mkuu wa CZ Information & Media Consultant LTD, Cyprian Majura Nyamagambile amesema kuwa anamshangaa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kukana hadharani kwamba hakumtuma Lowassa kwenda kuonana na Rais Dkt. Magufuli Ikulu,

Ameyasema hayo hii leo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa Mwenyekiti wa chama hicho ndiye aliyemshawishi Lowassa kwenda kuonana na Rais Magufuli.

“Namshangaa sana Mbowe kwa kumkana Lowassa kuhusu kwenda Ikulu kuonana na Rais, wakati yeye ndiye aliyemtuma akazungumze naye, sasa Chadema inabidi wamuangalie sana,”amesema Cyprian

Video: RC Makonda amsaidia Mjane aliyetapeliwa
JPM atuma salamu ajali iliyoua watu 11 Kagera